Zoezi la usajili wa wapiga kura imekamilika siku ya leo. Vituo kadhaa vya usajili wa wapiga kura nchini Kenya, vilikuwa na wakenya wengi waliokuwa kwenye harakati za mwisho, ili kutaka wasajiliwe.

Kwa upande mwingine, wakenya wengi waligadhabishwa kutokana na ukosefu wa vitambulisho ikiwa ni changamoto kubwa na muda mfupi wa usajili.

Hata hivyo, tume huru ya ujaguzi na maeneo ya mipaka IEBC, ilisema kuwa, haitaongeza muda wa kusajiliwa kwa wakenya, kama wapiga kura wapya, ambao hawajasajiliwa.