Waziri wa elimu Fred Matiang'i

Waziri wa Elimu Fred Matiang’i Jumanne amefichua kuwa kufikia sasa ni shule 68 ambazo zimekumbwa na machafuko ya ujambazi wa wanafunzi muhula huu.Amesema kuwa shule hizo zimeripoti visa vya ujambazi wa kila aina ukiwemo ule wa kuchoma mabweni.

Aidha, waziri huyo alisema kuwa kwa sasa anategemea idara ya mahakama iwe ya kwanza katika kusaidia hali hiyo kupata suluhu “kupitia kuwaadhibu vikali watuhumiwa wa visa hivyo.”

Waziri wa elimu Fred Matiang'i
Waziri wa elimu Fred Matiang’i