Bi Margret Kenyatta, ambaye ni mkewe rais Uhuru Kenyatta,Bi. Cecile Mbarire ambaye ni mbunge wa Runyenjes, na waziri wa vijana na jinsia Bi.Cecile Kariuki, waliweza kuungana na wakenya wengine katika siku ya wanawake duniani kwenye hafla iliyoandaliwa katika jumba la kimataifa la mikutano KICC, jijini Nairobi.

Aidha wabunge hao waliwataka wanawake waende mashinani, wapiganie viti vya ubunge ili kusimamia wanawake wengine bungeni.